www.vessella.it www.changamano.org
 

Cerca / Tafuta

Prima pagina / Ukurasa wa kwanza

Se vuoi essere informat@ sugli ultimi articoli pubblicati, iscriviti al nostro NOTIZIARIO, premendo sul pulsante.

Corso di swahili

Vocabolario italiano-swahili

Redazione

Pindupindu ?lapindua? watu 45 Jijini

2006-05-12


Mary Wejja

Tangu mvua zianze kunyesha mfululizo, idadi ya wagonjwa wa kipindupindu Jijini imeongezeka ambapo sasa wagonjwa wapya wako 45.

Taarifa ya tathmini ya ugonjwa wa kipindupindu iliyotolewa na Afisa Uhusiano wa Jiji, Bw.Gaston Makwembe imeonyesha kuna wagonjwa wapya katika Manispaa zote.

Taarifa imetaja baadhi ya maeneo ambayo wagonjwa hao wametokea kuwa ni Buguruni, Vingunguti, Ukonga,
Tabata, Ilala, Kiwalani, Kipawa, Kariakoo, Segerea, Kitunda, Chanika kwa Manispaa ya Ilala ambayo ina jumla ya wagonjwa 16.

Maeneo mengine ni Manzese, Mabibo, Kawe,Tandale, Kigogo, Kunduchi na Hananasifu kwa manispaa ya Kinondoni ambayo ina jumla ya wagonjwa 9.

Kwa upande wa Temeke, maeneo yenye wagonjwa ni Mbagala, Charambe, Tandika,Sandali,Chang'ombe,Yombo Vituka, Mji Mwema na Vijibweni ambapo jumla ya wagonjwa waliopo ni watano.

Aidha taarifa imebainisha kuwa kuna jumla ya wagonjwa 45 waliokuwepo,30 walioruhusiwa,69 waliolazwa na hakuna aliyefariki.

Hata hivyo manispaa za Jiji zimefanya jitihada za kufanya ukaguzi wa majengo 89, na vyoo 16.

Baada ya ukaguzi huo sehemu za biashara za chakula 20, za vinywaji 15, baa 5 na migahawa 4 zimeagizwa kuwekwa katika hali ya usafi kabla ya kuendelea kutoa huduma.

Aidha Mganga huyo ametoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kuchemsha maji ya kunywa, kuacha tabia ya kutiririsha maji kutoka vyooni na kufuata sheria za afya.

 

Il colera colpisce altre 45 persone in citt

2006-05-12


Mary Wejja

Prima che la pioggia iniziasse a cadere incessantemente, il numero degli ammalati di colera in citt? ? aumentato ed ora i nuovi ammalati sono 45.

Il bollettino sul colera emesso dall'Ufficiale di Relazione della Citt?, Sig. Gaston Makwembe, mostra che vi sono nuovi ammalati in tutte le municipalit?.

Il comunicato cita alcune zone in cui si sono verificati casi di colera: Buguruni, Vingunguti, Ukonga, Tabata, Ilala, Kiwalani, Kipawa, Kariakoo, Segerea, Kitunda, Chanika della Municipalit? di Ilala in cui vi sono 16 ammalati.

Altre zone sono: Manzese, Mabibo, Kawe, Tandale, Kigogo, Kunduchi e Hananasifu della Municipalit? di Kinondoni in cui vi sono 9 [24?] ammalati.

Per quanto riguarda Temeke, le zone con ammalati sono Mbagala, Charambe, Tandika, Sandali, Chang'ombe, Yombo Vituka, Mji Mwema e Vijibweni in cui vi sono cinque casi.

Inoltre il comunicato chiarisce che dei 45 ammalati, 30 sono stati dimessi, 69 sono stati ricoverati e nessuno ? morto [i conti non tornano!].

Comunque le municipalit? della metropoli si sono impegnate nell'ispezionare 89 costruzioni e 16 servizi igienici.

Dopo questa ispezione, a 20 punti vendita di cibo, 15 rivendite di bevande e 4 caff? ? stato ordinato di migliorare le condizioni igieniche prima di continuare a fornire servizio pubblico.

Inoltre il Dottore ha invitato i cittadini a prendere l'abitudine di far bollire l'acqua da bere, abbandonare l'abitudine di far scorrere l'acqua dai gabinetti e di seguire norme igieniche [pi? scrupolose].

( Nino Vessella)

Changamano ONLUS (www.changamano.org).

© Nino Vessella, 2003-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.