www.vessella.it www.changamano.org
 

Cerca / Tafuta

Prima pagina / Ukurasa wa kwanza

Se vuoi essere informat@ sugli ultimi articoli pubblicati, iscriviti al nostro NOTIZIARIO, premendo sul pulsante.

Corso di swahili

Vocabolario italiano-swahili

Redazione

Majambazi yafukua kaburi Dar.

2006-05-31


Sasa majambazi yamevuka mipaka. Baada ya kuona nyendo zake za kupora mabenki, maduka ya fedha za kigeni na kuteka nyara magari zimeshtukiwa, sasa yamehamishia mawindo yake kwingine kabisa ambako si rahisi kudakwa.

Ili kuwapoteza watu maboya, majambazi hayo hayakuhamishia mawindo yake kwenye maghala yanayotunza mali za thamani ama maduka ya jumla yaliyosheheni bidhaa za gharama.

Katika hali ya kushangaza, majambazi yameamua kwenda kufanya kufuru maeneo ambayo yanapaswa kuheshimiwa kutokana na kuhifadhi miili ya wapendwa wetu, maeneo ya makaburini.

Kundi la majambazi likiwa kamili kamili kupambana na yeyote ambaye angetibua dili lao, usiku wa kuamkia leo limevamia makaburi yaliyoko eneo la Kisauke nje ya kidogo ya Jiji.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili leo asubuhi zimedai kuwa majambazi hayo yalivamia makaburi usiku wa manane wakati watu wanaoishi jirani na maeneo hayo wakiwa wamelala fofofo.

Habari zaidi zimedai kuwa makaburi hayo yako kwenye shamba linalomilikiwa na familia moja inayoishi Jijini.

Imeelezwa kuwa huko shambani kuna mlinzi ambaye anaangalia mashamba na kwamba ndiye aliyetoa taarifa hizo kwa majirani zake.

Hata hivyo majirani hao hawakutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ingawa wamedai kuwa huenda wahalifu hao walitaka kupora vito vya thamani alivyozikwa navyo marehemu.

Gazeti hili linaendelea kufuatilia tukio hilo ili kupata undani wake.

 

Delinquenti dissotterrano tombe a Dar.

2006-05-31


Ora i delinquenti hanno oltrepassato i limiti. Dopo aver visto che gli abituali assalti di banche, di uffici dei cambi e le catture di automobili vengono colpiti, ora hanno trasferito la loro caccia in un posto completamente diverso e difficile da prendere.

Per confondere le acque, questi delinquenti hanno trasferito i loro bottini nei depositi che conservano gli oggetti di valore o presso i grossisti che immagazzinano merci costose.

Incredibilmente, i delinquenti hanno deciso di andare a dissacrare una zona che deve essere rispettata perch? conserva i corpi dei nostri cari, i camiteri.

Un gruppo di delinquenti pronti ad affrontare chiunque li avesse intralciati ieri notte ha invaso le tombe di Kisauke, poco fuori la citt?.

Le informazioni arrivate al giornale questa mattina affermano che questi delinquenti hanno invaso il cimitero a notte fonda, quando le persone residenti vicino alla zona dormivano profondamente.

Ulteriori notizie sostengono che le tombe si trovano in un campo di propriet? di una famiglia che vive in citt?.

E' stato spiegato che nel campo c'? una guardia che lo sorveglia e che ? stata proprio lei a informare i vicini.

Tuttavia i vicini non hanno fornito ulteriori informazioni sull'accaduto sebbene abbiano dichiarato che forse questi criminali volevano rubare gli oggetti di valore con cui sono stati sepolti i defunti.

Questo giornale continuer? a indagare a fondo su questo episodio.

( Nino Vessella)

Changamano ONLUS (www.changamano.org).

© Nino Vessella, 2003-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.