WWF yawasha moto kupambana na kilimo cha 'vinyungu' bonde la Rufiji
2006-05-27
Johnson Mbwambo
Mzee Muze Leokasi ni mkulima mdogo wa miaka mingi katika kata ya Bomang'ombe, wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.
Mzee huyo haelewi ni kwa nini anakatazwa kulima karibu na kingo za mto katika shamba lake lililoko bondeni, wakati akilima anapata mazao mengi kuliko akilima katika maeneo ya mlimani.
'Nikilima shamba langu la bondeni karibu na mto navuna viazi mara tano zaidi kuliko ninavyovuna mlimani kwenye shamba langu lingine la ukubwa huo huo,' Mzee Muze aliuamabia ujumbe wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) uliotembelea kijiji hicho, hivi karibuni.
Hata hivyo, asichokijua mzee huyo ni kwamba kwa kadri shamba lake hilo, na ya wenzake yanavyokaribia kingo za mto; ndivyo pia wanavyouweka mto huo katika hatari ya kukauka na kutoweka kabisa katika ramani ya kijiji chao.
Na kwa kuwa maji ya mto huo yanatiririka na kupita katika vijiji vingine, kilimo chao hicho ni 'maafa' kwa vijiji vingine.
'Furaha' yao hiyo ya muda ndiyo maafa ya wenzao katika vijiji vingine.
Katika bonde la Rufiji, kilimo hicho katika vyanzo vya maji na kwenye kingo za mito na mifereji kinajulikana kama 'kilimo cha vinyungu'.
Mzee Muze ni mmoja wa maelfu ya wakulima wadogo katika bonde la Rufiji ambao Shirika la Mazingira Duniani (WWF) limepania kupambana nao kwa kuwaelemisha jinsi kilimo cha 'vinyungu' kinavyochangia katika kuteketeza vyanzo vingi vya maji.
WWF inaifanya kazi hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wake wa miaka mitano wa Ruaha Water Programme.
Haijulikani kilimo hicho cha 'vinyungu' kilianza lini hasa katika bonde la Rufiji.
Wako wanaodai kilikuwepo hata enzi za ukoloni; lakini wako wengine wanaoamini kuwa kilianza katika miaka ya sabini.
Hata hivyo, karibu wataalamu wote wa kilimo wanakubaliana kwamba kilianza kupamba moto katika miaka ya tisini.
Kutokana na kuchoka na kuishiwa rutuba kwa ardhi katika maeneo ya milimani na pia kwa sababu ya ukame, wakulima walianza kuhamia mabondeni wakati wa kiangazi na kupanda mbegu za maboga zilizoitwa 'kinyungu', .
Hapo ndipo kilimo hicho cha mabondeni kilipopachikwa jina la kilimo cha 'vinyungu'; yaani kilimo cha maboga.
Ingawa kilimo hicho kilianza kwa kupanda maboga (tena wakati wa kiangazi tu), baadaye kilihusisha mazao mengine kama vile mahindi, viazi na hata njegere.
Aidha, badala ya kulimwa nyakati za kiangazi tu, kama ilivyokuwa awali, sasa kinafanyika katika misimu yote; hata wakati wa masika ambao, angalau, una mvua za kutosha.
Kwa mujibu wa Ofisa wa WWF, anayesimamia mradi wa maji wa bonde hilo Bw. Petro Masolwa, kilimo hicho cha 'vinyungu' kimechangia mno katika kutoweka kwa vyanzo vingi vya maji katika bonde hilo, hasa katika Mikoa ya Mbeya na Iringa.
'Watu wanajiuliza nini kinasababisha mtiririko mdogo wa maji katika The Great Ruaha River. Ukweli ni kwamba kilimo kisicho endelevu hasa hiki cha 'vinyungu' ndicho kinachosababisha hali hiyo. Bonde la Rufiji lina watu karibu milioni tatu,' anasema Bw Masolwa.
Katika ziara hiyo ya JET, maofisa wa WWF waliwatembeza waandishi wa habari katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Kilolo na Iringa Vijijini, kuona mafanikio ya juhudi walizozifanya katika kupambana na kilimo hicho kibaya.
'Kumbe sasa tumewajua wanaolikausha bwawa la Mtera,' ndiyo iliyokuwa kauli ya mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi, Lugano Mbwina, aliyoitoa katika kijiji cha Kidabaga, baada ya kuona shamba la mkulima mmoja aliyelima karibu kabisa na kingo ya mkondo wa mto.
Mafanikio makubwa ya mradi huo yalionekana katika wilaya ya Kilolo ambako, kutokana na elimu iliyotolewa, wananchi wana mwamko mkubwa mno wa kupambana na wakulima wanaolima karibu na kingo za mito/mifereji au karibu kabisa na vyanzo vya maji.
'Wakati wa kuwaelemisha, hatukuwaambia waache kabisa kulima mabondeni, hatukuwaambia waache kabisa kilimo cha 'vinyungu', lakini tuliwaambia mashamba yao yawe umbali wa kati ya mita tatu na 15 kutoka katika kingo ya mto au mfereji au chanzo chochote cha maji', alisema Mratibu wa Mpango wa Kuhifadhi Maeneo Bonde Kilolo, Bw Makungu Lubegili.
'Wilaya ilianza kwanza kwa kutafiti maeneo yanayokubalika kuwa ni vyanzo vya maji, na tulipata maeneo 210 ambayo yote ni mabonde,' alisema Bw Lubegili na kuongeza ' baada ya hapo wilaya ilifanya kazi ya kutambua mabonde yaliyoathirika na kilimo hicho cha 'vinyungu' na baada ya kuyajua ndipo utekelezaji wa programu ulipoanza.'
Kwa mujibu wa Bw Lubegili, programu hiyo inahusisha vijiji 18 katika wilaya hiyo.
"Tuliendesha mafunzo vijijini, tukafanya mikutano ya hadhara na hatimaye wananchi wakawa na mwamko na sasa tunawashirikisha katika programu hiyo ya kulinda vyanzo vya maji," alisema.
Matokeo ya juhudi hizo ni kwamba sasa wakulima hawalimi tena karibu kabisa na vyanzo vya maji, na wale wanaokaidi huchukuliwa hatua kwa kufuata sheria ndogo ndogo zilizopitishwa nao wenyewe wananchi.
Kauli ya ofisa huyo inaungwa mkono na mkulima wa kijiji cha Kidabaga, Bi Angelina Mlovelwa ambaye aliuambia ujumbe huo wa JET: 'baada ya elimu kutolewa wananchi wamekubali kuacha mita tatu, tano au hata kumi na tano kutoka katika kingo.
Mita za kuacha hutegemea ukubwa wa mto wenyewe au mfereji.'
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kidabaga, Amini Tengelakwi anasema ya kuwa ardhi milimani imechoka na ndiyo sababu wanavijiji waliamua kuvamia ardhi ya maeneo ya bondeni ambayo ina rutuba na ni nyevunyevu.
Kauli hiyo ya uchovu wa ardhi ya milimani inaungwa mkono na Lubegili ambaye pia anasema kuwa, ni muhimu wanavijiji wakafundishwa pia mbinu bora za kulima katika maeneo ya milimani kama vile kilimo cha matuta.
Bw Lubegili na WWF, wanaamini, hata hivyo, kwamba wakulima wakiendelea kuacha kulima mita tatu , tano au 15 kutoka kingo za mito/mifereji au vyanzo vingine vya maji, ni dhahiri maji yataongezeka, na hivyo mashamba yao yatakuwa chepechepe kiasi kwamba watalazimika kurudi nyuma.
'Maji yatawasukuma nyuma mpaka kwenye mwanzo wa milima waliyoikimbia. Na kwa sababu hiyo, ni lazima wazikubali mbinu za kuendesha kilimo endelevu cha mashamba yaliyo milimani,' alisema Lubegili.
Kwa mtazamo wa WWF, na kwa hakika, mtazamo wa wanamazingira wote, mradi huo utasaidia mno kuongeza viwango vya maji katika mito mikubwa ya bonde la Rufiji ambayo baadhi yao ni muhimu mno katika uzalishaji umeme nchini.
'Viwango vya maji vya mito hiyo vitakuwa vikubwa kwa sababu vyanzo vyake vitakuwa vinalindwa. Katika hali hio, tunaweza kusahau kabisa masuala ya mgao wa umeme,' alisema.
Lakini mradi huo wa WWF wa maji katika bonde la Rufiji haujihusishi tu na mapambano dhidi ya kilimo hicho cha 'vinyungu'; lakini pia shughuli nyingine zinazolenga kuwakomboa wakulima wadogo wadogo kutoka katika umasikini.
Shughuli hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOSA), kuanzishwa kwa Vyama vya Wakulima na Watumiaji Maji na pia katika sekta ya elimu ambako husaidia shule.
Mradi huo ulioanza Julai 2003 na unaotarajiwa kumalizika mwaka 2008 unaendeshwa kutokana na pesa za ufadhili wa ofisi ya WWF nchini Uingereza (WWF UK).
Malengo ya mradi huo ni kwamba ifikapo mwaka 2,010 wakulima waishio maeneo ya bonde katika wilaya nane zilizomo katika bonde la Rufiji, watakuwa na mipango madhubuti ya usimamizi na matumizi endelevu ya raslimali ya maji.
*Johnson Mbwambo ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).
|
|
WWF accende la lotta alla coltura di 'zucche' nella valle del Rufiji
2006-05-27
Johnson Mbwambo
Il Sig. Muze Leokasi ? un anziano piccolo contadino della circoscrizione di Bomang'ombe, distretto di Kilolo, regione di Iringa.
Questo signore non capisce perch? gli ? vietato coltivare vicino alle rive del fiume nel suo campo che si trova nella valle, mentre se vi coltivasse avrebbe molto pi? raccolto che nelle zone collinari.
"Se coltivassi il mio campo a valle vicino al fiume raccoglierei patate cinque volte pi? di quanto raccolgo in collina nell'altro campo della stessa grandezza," ha detto il sig. Muze al rappresentante dell'Associazione dei Giornalisti di Questioni Ambientali della Tanzania (JET [Journalists Environmental Association of Tanzania]) che ha recentemente visitato il villaggio.
Tuttavia, quello che questo signore non sa ? che quanto pi? il suo campo e quello dei suoi amici si avvicinano alle rive del fiume, tanto pi? mettono questo fiume in pericolo di prosciugamento e di cancellazione dalla mappa del loro villaggio.
E poich? l'acqua del fiume scorre attraverso altri villaggi, la loro coltivazione ? una 'calamit?' per gli altri villaggi.
Questa loro "felicit?" temporanea ? la disgrazia dei loro amici di altri villaggi.
Nella vallata del Rufiji, la coltivazione nelle sorgenti d'acqua e presso le rive di fiumi e altri corsi d'acqua ? nota come "coltivazione di zucche".
Il sig. Muze ? uno delle migliaia di piccoli contadini della valle del Rufiji che il Fondo Mondiale per la Natura (WWF) intende affrontare per istruirli su come la coltivazione di "zucche" contribuisce a distruggere molte sorgenti d'acqua.
Il WWF svolge questo lavoro come parte del suo piano quinquennale del Ruaha Water Programme.
Non si sa esattamente quando questa coltivazione di "zucche" sia iniziato nella valle del Rufiji.
Alcuni dicono che c'era perfino durante il periodo coloniale, ma altri credono che sia iniziata negli anni settanta.
Tuttavia, quasi tutti gli esperti di agricoltura concordano sul fatto che sia divampata negli anni novanta.
Per l'affaticamento e l'esaurimento dell'humus del terreno della zona collinosa e anche per la siccit?, i contadini hanno cominciato a trasferirsi nella valle durante la stagione secca e a piantare semi di zucche chiamate 'kinyungu'.
E' allora che a questa coltivazione valliva ? stato affibbiato il nome di coltivazione di "vinyungu"; cio? coltivazione di zucche.
Sebbene questa coltivazione sia iniziata con le zucche (e solo nella stagione secca), dopo ha riguardato altri prodotti come granturco, patate e perfino piselli.
Inoltre, invece di essere fatta soltanto nei periodi secchi, come era prima, ora viene effettuata in tutte le stagioni; perfino durante le stagioni che hanno pioggia a sufficienza.
Secondo il funzionario del WWF, che dirige il progetto dell'acqua della valle, Sig. Petro Masolwa, la coltivazione di "zucche" contribuisce molto nella distruzione delle fonti d'acqua della valle, soprattutto nelle regioni di Mbeya e Iringa.
"Le persone si chiedono cosa causa il poco flusso d'acqua del The Great Ruaha River. La verit? ? che proprio la coltivazione non moderna, soprattutto questa di 'zucche', provoca questa situazione. La valle del Rufiji ha circa tre milioni di persone,' dice il Sig. Masolwa.
In questo viaggio della JET, i funzionari del WWF hanno accompagnato i giornalisti in alcuni villaggi della provincia di Kiloro e Iringa Vijijini, a vedere gli sforzi fatti nel contrastare questa cattiva coltura.
"Caspita, ora sappiamo chi ? che prosciuga il bacino di Mtera,' questa ? stata l'affermazione del giornalista di Mwananchi, Lugano Mbwina, all'uscita dal villaggio di Kidabaga, dopo aver visto il campo di un contadino che coltivava vicinissimo alla riva del corso del fiume.
Grandi successi di questo programma si sono visti nella provincia di Kilolo, dove, per l'istruzione data, gli abitanti hanno una grande consapevolezza nella lotta ai contadini che coltivano vicino alle rive dei fiumi o corsi d'acqua o vicino alle sorgenti.
"Nel periodo di addestramento, non abbiamo detto loro di abbandonare completamente la coltivazione a valle, non abbiamo detto loro di abbandonare completamente la coltura di 'zucche', ma abbiamo detto loro che i campi dovevano essere a una distanza fra 3 e 15 metri dalla riva del fiume o corso d'acqua o una sorgente", ha dichiarato l'Ispettore del Programma di Conservazione della Zona Valliva di Kilolo, Sig. Makungu Lubegili.
"Il distretto ha iniziato con una ricerca delle zone riconosciute come sorgenti e abbiamo trovato 210 aree tutte nella valle," ha detto il sig. Lubegili e ha aggiunto "dopo il distretto ha fatto il lavoro di individuazione delle valli influenzate da questa coltura di "zucche" e dopo averle riconosciute ? iniziata la realizzazione del piano."
Secondo il Sig. Lubegili, il programma riguarda 18 villaggi di questo distretto.
"Abbiamo condotto i corsi nei villaggi, e abbiamo fatto incontri pubblici e alla fine gli abitanti avevano acquistato consapevolezza e ora li facciamo partecipare al programma di protezione delle sorgenti," ha detto.
I risultati di questi sforzi sono che ora i contadini non coltivano pi? a ridosso delle sorgenti, e per quelli che osano farlo si prendono le misure previste dai regolamenti approvati dai cittadini stessi.
L'affermazione di questo funzionario ? confermata dalla contadina del villaggio di Kidabaga, Sig.ra Angelina Mlovelwa, che ha detto al rappresentante del JET: "dopo l'insegnamento ricevuto i cittadini hanno accettato di lasciare tre, cinque e perfino quindici metri dalla riva.
I metri da lasciare dipendono dalla grandezza del fiume stesso o del corso d'acqua."
Il funzionario esecutivo del villaggio di Kidabaga, Amini Tengelakwi, ha detto che il terreno collinare ? esaurito ed ? per questo che gli abitanti dei villaggi hanno invaso le zone vallive che sono fertili e umide.
Questa affermazione sull'esaurimento del terreno collinare ? sostenuta da Lubegili che aggiunge che ? importante per gli abitanti del villaggio essere istruiti anche sulle tecniche migliori di coltivazione nelle zone collinari come, per esempio, la coltura a porche.
Il Sig. Lubegili e il WWF credono, tuttavia, che se i contadini continuano a lasciare tre, cinque o quindici metri dalle rive dei fiumi o corsi d'acqua o altre sorgenti, ? chiaro che l'acqua aumenter? e cos? i loro campi saranno tanto bagnati da obbligarli a tornare indietro.
"L'acqua li spinger? indietro fino all'inizio delle colline da cui sono fuggiti. E perci? devono accettare le tecniche della coltivazione moderna dei campi che sono in collina," ha detto Lubegili.
Dal punto di vista del WWF, e per certo, di tutti gli ambientalisti, questo progetto aiuter? molto ad aumentare la quantit? d'acqua dei grandi fiumi della valle del Rufiji, di cui molti sono molto importanti per la produzione di elettricit? per il paese.
"Le quantit? d'acqua di questi fiumi saranno grandi perch? le loro sorgenti saranno protette. In questa situazione possiamo dimenticare completamente la questione della distribuzione di elettricit?," ha dichiarato.
Ma il progetto del WWF dell'acqua nella valle del Rufiji non riguarda soltanto la lotta contro questa coltura di "zucche", altre iniziative hanno l'obiettivo di riscattare i piccoli contadini dalla povert?.
Queste iniziative riguardano la costituzione di Associazioni degli Investimenti e dei Prestiti, delle Associazioni dei Contadini e degli Utilizzatori delle acque e anche il settore dell'istruzione, con aiuti alle scuole.
Questo progetto iniziato nel luglio 2003 e che si prevede debba terminare nel 2008 ? finanziato dall'ufficio del WWF inglese (WWF UK).
Secondo gli obiettivi di questo progetto nel 2010 i contadini che vivono nelle zone vallive degli otto distretti della valle del Rufiji, avranno solidi piani di gestione e uso moderno delle risorse d'acqua.
*Johnson Mbwambo ? il Segretario Generale dell'Associazione dei Giornalisti di Questioni Ambientali della Tanzania (JET).
(
Nino Vessella)
|