Polisi Dodoma wameteketeza ekari mbili na nusu za mashamba ya bangi
2006-05-31
Polisi mkoani Dodoma wameteketeza ekari mbili na nusu za mashamba ya bangi katika milima ya kijiji cha Chololo kilichopo wilayani Kongwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Bwana Omary Mganga amesema mashamba hayo yalikuwa yanamilikiwa na wakazi wawili wa kijiji hicho Titus Sabugo, na Abineli Mbumi ambao wamekimbia kabla hawajatiwa nguvuni.
Kamanda Mganga amesema katika msako unaoendeshwa na jeshi la polisi mkoani humo wa kuteketeza mashamba ya bangi, kuwasaka majambazi na watu wanaomiliki silaha kinyume na sheria, wamefanikiwa kuwakamata silaha mbili aina ya gobore.
|
|
La polizia di Dodoma distrugge due ettari e mezzo di oppio
2006-05-31
La polizia della regione di Dodoma ha distrutto due ettari e mezzo di campi di oppio nelle colline del villaggio di Chololo, nel distretto di Kongwa.
Il comandante della polizia della regione di Dodoma, Sig. Omary Mganga, ha detto che questi campi erano di propriet? di due abitanti del villaggio, Titus Sabugo e Abineli Mbumi, che sono fuggiti prima di essere messi in carcere.
Il Comandante Mganga ha detto che durante la retata condotta dai poliziotti nella regione per distruggere i campi di oppio, hanno catturrato malavitosi e persone in possesso di armi illegali, sono riusciti a catturrare due armi del tipo ad avancarica.
(
Nino Vessella)
|