www.vessella.it www.changamano.org
 

Cerca / Tafuta

Prima pagina / Ukurasa wa kwanza

Se vuoi essere informat@ sugli ultimi articoli pubblicati, iscriviti al nostro NOTIZIARIO, premendo sul pulsante.

Corso di swahili

Vocabolario italiano-swahili

Redazione

'Msife moyo mtalipwa na Mungu'

2006-05-31


Futuna Seleman

Serikali imewapa moyo walimu wakuu wa shule za msingi zilizopo Jijini ikisema licha ya mshahara kiduchu wasife moyo kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu watapata hifadhi kwa kwenda peponi.

'Walimu tunaomba msige moyo... zaidi ya mshahara tunapata hifadhi kwa Mungu naamini pepo inatungoja maana hakuna anayekuwa mwana taaluma bila kupitia kwa mwalimu...maprofesa wahandisi, waandishi wa habari, madaktari bingwa wote lazima wafundishwe na walimu,' akasema Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi Bi Mwantumu Mahiza.

Naibu Waziri huo alikuwa akifunga mkutano wa shirikisho la Walimu wa Shule za msingi za Afrika Mashariki.

Amesema hata kama mwalimu akipewa mshahara wa shilingi milioni moja, pesa hiyo ni kiduchu pasipo kuboresha miundo mbinu kwa walimu hao.

Amewaomba walimu hao kuvuta subira licha ya kero sugu zinazowakabili kwa vile kwa sasa Serikalia inaangalia uzito wa mazingira hayo na namna ya kuyatatua kwa kutumia tume iliyoundwa kushughulikia maslahi ya watumishi wa umma.

 

'Non disperate, sarete ripagati da Dio'

2006-05-31


Futuna Seleman

Il governo incoraggia i direttori delle scuole elementari della Citt? dicendo che nonostante l'irrisorio stipendio non devono disperarsi perch? avranno da Dio Onnipotente la sicurezza del paradiso.

"Chiediamo agli insegnanti di non disperare... oltre allo stipendio abbiamo la protezione di Dio, credo che il paradiso ci aspetti perch? non c'? nessuna persona istruita che non abbia avuto un insegnante... professori, ingegneri, giornalisti, esperti dottori, tutti devono essere istruiti dagli insegnanti,' ha detto il Vice Ministro dell'Istruzione e della Professionalit?, Sig.ra Mwantumu Mahiza.

Il Vice Ministro stava chiudendo l'incontro della federazione degli Insegnanti di Scuola Elementare dell'Africa orientale.

Ha detto che anche se l'insegnante ricevesse uno stipendio di un milione di scellini [circa 1000 euro], questo denaro sarebbe insignificante senza un miglioramento strutturale degli insegnanti.

Ha chiesto agli insegnanti di pazientare con le loro croniche difficolt?, perch? ora il Governo sta esaminando la gravit? di questa situazione e la maniera di risolverla grazie ad un comitato appositamente costituito per occuparsi dello stato generale dei dipendenti pubblici.

( Nino Vessella)

Changamano ONLUS (www.changamano.org).

© Nino Vessella, 2003-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.