www.vessella.it www.changamano.org
 

Cerca / Tafuta

Prima pagina / Ukurasa wa kwanza

Se vuoi essere informat@ sugli ultimi articoli pubblicati, iscriviti al nostro NOTIZIARIO, premendo sul pulsante.

Corso di swahili

Vocabolario italiano-swahili

Redazione

Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi kwanza

2009-06-24


TUKIWA chombo kinachotetea haki, wajibu na uhuru wa umma katika kuchagua viongozi na kuamua mustakabali wa taifa, tunachukua fursa hii kwa moyo wa shaka, kuelezea hofu yetu juu ya kauli ya serikali, kwamba kuanzia sasa Mpigachapa Mkuu wa Serikali ndiye atakayekuwa anachapa nyaraka zitakazotumika katika upigaji kura nchini.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitoa kauli hiyo juzi bungeni wakati akisoma hotuba ya makadirio na matumizi ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na kufafanua uamuzi huo.



Mosi, alisema utaratibu huo utaanza kutumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.



Kwamba Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 itafanyiwa marekebisho kuondoa vipengele vya sheria hiyo vinavyoruhusu takrima katika uchaguzi, na kuandaa vigezo na utaratibu utakaotumika kugawa majimbo ya uchaguzi nchini.



Marekebisho hayo yataongeza muda wa kufungua kesi za kupinga matokeo na kuweka kikomo cha mgombea kujitoa katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupewa mamlaka ya kuandikisha wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa na kipindi maalum cha kuboresha daftari la wapiga kura, walau mara mbili kati ya uchaguzi mmoja kwenda mwingine.



Kimsingi, maamuzi yote hayo ya serikali yanaonekana kuwa na manufaa kwa taifa, hususan katika kupunguza gharama zitokanazo na mchakato wa uchaguzi.



Pia, uamuzi wa kuifanyia marekebisho Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985, hususan katika kuongeza muda wa kufungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi, kuweka kikomo cha mgombea kujitoa katika uchaguzi, na kuondoa vipengele vinavyoruhusu takrima, ni uamuzi wa busara unaopaswa kuungwa mkono na Mtanzania yeyote anayejali ushindani bora na wa haki katika mfumo wetu wa siasa za vyama vingi.



Hata hivyo, bado tuna hofu na maamuzi hayo ya serikali hususan kumfanya Mpigachapa Mkuu kuwa mchapaji wa nyaraka za uchaguzi.



Tunaamini kuwa maamuzi hayo yalipaswa kutanguliwa kwanza na marekebisho ya muundo na mfumo mzima wa uundaji na utendaji kazi wa NEC, kwani inaweza kuendelea kutumiwa vibaya kulinda maslahi ya chama kilicho madarakani badala ya kulinda maamuzi ya umma.



Msingi wa hofu yetu unatokana na ukweli kuwa, Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali, sawa na NEC, nayo haitakuwa na uhuru wa kufanya kazi hiyo kwa uadilifu, kwani kama sehemu ya serikali, kuna wakati italazimika kutumiwa vibaya na viongozi wa serikali wa chama kilicho madarakani (chochote kile), kuhakikisha kuwa inatekeleza njama fulani ya kuhakikisha kinashinda uchaguzi, hata kama ushindi huo hautakuwa na ridhaa ya umma.



Vivyo hivyo, vipengele vingine vyote vinavyokusudiwa kurekebishwa katika Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985, pamoja na umuhimu wake, bado havina uhakika wa kutekelezeka au kuheshimiwa hasa na chama kinachokuwa madarakani, ikiwa hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi, itakayosimamia kwa haki sheria na taratibu halali za uchaguzi, baada ya marekebisho hayo.



Kwa hiyo, tunaitaka serikali kwa kushirikiana na wadau wote wa siasa za vyama vingi, kuanza kwanza kuiunda upya NEC ili iwe na muundo na mfumo ulio huru zaidi katika kutekeleza majukumu yake, utakaoaminiwa na wadau wote nchini na kulinda haki na uhuru wa raia katika kuamua viongozi wao na mustakabali wa taifa lao.

 

Prima di tutto vogliamo una Commissione Elettorale Indipendente.

2009-06-24


Poiché siamo lo strumento che difende i diritti, i doveri e la libertà del popolo nella scelta dei dirigenti e nelle decisioni del futuro della nazione, cogliamo l'occasione con animo dubbioso, per spiegare i nostri timori riguardo alla decisione del governo di affidare proprio alla Tipografia di Stato la stampa dei documenti da usare nelle elezioni nel paese.


Il Primo Ministro, Mizengo Pinda, lo ha annunciato l’altro ieri in Parlamento mentre presentava le stime e le spese del bilancio preventivo del suo ufficio per l'anno finanziario 2009/2010 e ha spiegato questa decisione.


Per prima cosa, ha detto che questa procedura inizierà ad essere utilizzata nelle elezioni dei governi dei quartieri che si svolgeranno alla fine di quest’anno e con le elezioni generali che si svolgeranno l’anno prossimo.


Ha detto che la Legge Elettorale del 1985 sarà modificata per eliminare i suoi articoli che permettono i festini nelle elezioni, e per preparare i criteri e le procedure che saranno utilizzati per istituire i distretti elettorali nel paese.


Queste modifiche allungheranno l'arco di tempo per impugnare i risultati e tenere in sospeso il candidato uscito dalle elezioni, poiché la Commissione Elettorale Nazionale (NEC), oltre a ricevere l’autorità di far registrare tutti gli elettori della Repubblica Unita della Tanzania, avrà un periodo speciale per aggiornare il registro degli elettori, almeno due volte fra un’elezione e un’altra.


Fondamentalmente, tutte queste decisioni del governo sembrano essere utili alla nazione, specialmente nel contenere i costi che si hanno durante lo svolgimento delle elezioni.


Inoltre, la decisione di modificare la Legge Elettorale del 1985, specialmente nell’aumentare l'arco di tempo impugnare i risultati elettorali, nel sospendere il candidato uscito dalle elezioni, di cancellare gli articoli che permettono i 'festini' [vd. nota], è una saggia decisione che deve essere sostenuta da qualsiasi tanzaniano che a cuore una vittoria vera e giusta nel nostro sistema politico multipartitico.


Nonostante ciò, abbiamo ancora timore di queste decisioni governative, specialmente quella di far diventare la Tipografia di Stato lo stampatore dei documenti elettorali.


Crediamo che queste decisioni sarebbero dovute essere precedute dalle modifiche al sistema e all'intera struttura di nomina e lavoro della Commissione Elettorale Nazionale (NEC), perché essa può continuare a essere usata male per difendere gli interessi del partito al potere invece di difendere le decisioni del popolo.


Il nostro timore si basa sul fatto che il Dipartimento della Tipografia di Stato, come la Commissione Elettorale Nazionale, non sarà libero di lavorare con rettitudine, perché come parte del governo, c’è un periodo che sarà costretto a lavorare male dai leader al governo del partito (qualunque esso sia) al potere, di accertare che non c'è stato qualche imbroglio per assicurargli la vittoria alle elezioni anche se questa vittoria non accontenterà del popolo.


In questo modo, tutti gli articoli della Legge Elettorale del 1985, con la sua importanza, che sono destinati a essere modificati dopo queste modifiche non hanno ancora la certezza di essere applicati o rispettati specialmente dal partito al potere, se non ci sarà una commissione indipendete d’inchiesta, che controlli con giustizia la legge e la legalità delle elezioni.


Perciò, vogliamo che il governo assieme a tutti i responsabili al sistema multipartitico, inizi dapprima a costituire ex-novo la Commissione Elettorale Nazionale (NEC) affinché abbia un sistema e una struttura che sia più; libera nell’adempiere le sue responsabilità, che sia credibile da tutti i responsabili del paese e che protegga il diritto e la libertà dei cittadini nello scegliere i loro leader e il futuro della loro nazione.


Nota: ricevimenti che i candidati danno in campagna elettorale e in cui distribuiscono piccole somme di denaro agli elettori, per assicurarsi il loro voto!

( Giovanna Fiorlenza [Nino Vessella])

Changamano ONLUS (www.changamano.org).

© Nino Vessella, 2003-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.