Vijiji kunufaika na umeme wa upepo
2009-05-24
Adam Malinda
TANZANIA inahitaji mbinu mbadala ili kuondosha tatizo la ukatikaji umeme ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Nchi yoyote duniani ili uchumi ukue ni lazima nishati ya umeme iwe ya uhakika, ndiyo maana nchi za Ulaya kwa kiasi kikubwa zimeondokana na umeme wa kufua unaotokana na maporomoko ya maji badala yake wamewekeza katika mashamba ya vinu vya kufua umeme kwa njia ya upepo ambao ni wa gharama nafuu.
Licha ya umeme wa upepo kuwa na gharama ndogo za uendeshaji, ni rafiki mkubwa wa mazingira, kwani hauhitaji nyenzo nyingine zaidi ya upepo wenyewe.
Umeme huu ni tofauti na ule unaozalishwa kwa jenereta kubwa zinazosababisha moshi mwingi wenye kemikali na kuharibu anga na kusababisha tabia joto duniani.
Hali ya ukosefu wa umeme wa uhakika nchini ni tatizo ambalo kila mmoja linamgusa katika kudhoofisha shughuli zake za kila siku, hapo ndipo tunapoitupia lawama serikali na kuitaka ipate njia mbadala ya kuondosha tatizo hili.
Akizunmgumza na Tanzania Daima katika ofisi zake zilizopo vingunguti jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Windpower Technics Tanzania, Amos Makele, anasema wamejizatiti kusambaza teknolojia ya umeme wa upepo nchini.
Makele anasema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2008, ingawa kabla ya hapo ilifanya utafiti wa kijiografia miaka minne kabla ili kukidhi viwango vinavyohitajika katika teknolojia ya umeme wa upepo.
Anasema mahitaji ya umeme kwa Watanzania ni makubwa kiasi, kwa hiyo kutumia umeme wa aina moja pekee ni kuchelewesha maendeleo kwa nchi changa kama Tanzania.
"Nchi za Ulaya na Marekani zimeachana kuwa tegemezi na umeme wa maporomoko ya maji badala yake wamerahisisha kwa kufua umeme wa upepo...na sisi Tanzania tunatakiwa tubadilike tuige mfano huo," anasema Makele.
Mtazamo wao anasema ni kufikisha huduma hiyo wilayani na vijijini ambako huduma ya umeme haijafika na hivyo kuwapa wepesi wananchi kuendesha shughuli zao katika maisha ya kisasa, ambapo umeme wao utakuwa ukifanyiwa matengenezo madogo madogo kwa vifaa vidogo kama betri.
"Hiyo betri utakapofungiwa, kinu chetu cha kufua umeme itakuchukua miaka 6 hadi 10 kukikagua," anasema mkurugenzi huyo.
Anabainisha kuwa umeme wa upepo hutumika katika maeneo mbalimbali katika nchi za Ulaya na Marekani kama vile barabarani mashambani, viwandani na viwanja vya michezo, kwa kuwa gharama zake ni nafuu ikilinganishwa na umeme wa aina yoyote duniani.
"Teknolojia hii haihitaji nyaya nyingi, haitumii aina yoyote ya mafuta ya mitambo, panga lake linapozungushwa na upepo hufua umeme unaoenda moja kwa moja katika kifaa kinacho itwa ‘inverter,’ hiki kinakuza umeme kadiri ya uwezo ulivyopangwa.
"Ndani ya kifaa hiki kuna fyuzi inayolinganisha kiwango cha umeme na kuupitisha kwenye kifaa kinachodhibiti hitilafu ya umeme," anasema Makele.
Makele anasema lengo la mradi wa ufuaji umeme wa upepo, limeitazama jamii ya Kitanzania hasa vijijini, kwani wamegundua kuwa wakazi wa vijiji wanakosa taarifa mbalimbali za kimaendeleo kupitia katika vyombo vinavyotumia umeme, hali inayowaathiri kiuchumi.
Anasema endapo wakazi wa vijijini watafikiwa na umeme, wataweza kusindika mazao yao baada ya kuvuna na kuyauza kwa bei kubwa, tofauti na kuuzwa kabla ya kusindikwa.
Lakini pia anasema vijijini watapa fursa ya kuuza vinywaji baridi.
Akizungunzia uwezo wa umeme wa upepo anasema una viwango tofauti kutegemea kinu cha ufuaji chenye ukubwa gani.
Akitolea mfano, anasema upo umeme wa ‘Watts 500, 1,000 na hata Megawatts 3,000,’ kutegemea shughuli zinazokusudiwa.
"Kama ni matumizi madogo ya taa, redio na televisheni, watts 500 zinatosha...ikiwa unahitaji kwa ajili ya friji inamlazimu mtumiaji awe na watts 1,000...lakini kwa shughuli za viwanda inamlazimu awe na shamba atakalozalisha ‘megawatts’ kadhaa ili apate umeme wa uhakika usiokuwa na mgawo wala bili za kila mwezi," anasema.
Makele anasema nia ya kuelekeza nguvu zao vijijini ni kuungana na juhudi za serikali za kuwafikishia huduma ya nishati ya umeme vijijini ili kurahisisha ukuaji wa uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja ama vikundi.
Anasema siku za hivi karibuni wameanza kwenda mikoani ya Dodoma, Singida, Shinyanga na Mwanza kwa ajili ya kusambaza huduma hiyo, ambapo baadaye watasambaza katika visiwa vya Ukara, Ukerewe, Saanane na vinginevyo, lengo likiwa ni kuwakomboa wakazi wa vijijini ambao wengi wao hutumia jenereta zinazowagharimu pesa nyingi.
Pamoja na hayo, Makele anaishauri serikali kuzipa ruzuku kampuni za uzalishaji wa nishati ya umeme ili kuwa na wepesi wa usambazaji vijijini ingawa ipo Mamlaka ya Nishati Vijijini (REA).
Makele anasema teknolojia hiyo si ya kupuuza kwani serikali ikidhamilia inaweza kuanzisha shamba kubwa la vinu vya kufua umeme wa upepo na kuzalisha megawati nyingi zinazoweza kuunganishwa katika gridi ya taifa na kukomesha tatizo la umeme na mgawo kwisha kabisa nchini.
|
|
L'utilità dell'energia eolica per i villaggi
2009-05-24
Adam Malinda
La Tanzania necessita di una strategia alternativa per risolvere il problema dell'interruzione dell’energia elettrica per poter accelerare lo sviluppo economico.
In tutti i paesi nel mondo, per far crescere l’economia è necessario che l’energia elettrica sia una assicurata, per questo i paesi Europei hanno in gran parte eliminato l’elettricità ricavata dalle cascate investendo, invece, nelle pale eoliche per ricavare elettricità dal vento che è una spesa vantaggiosa.
L’energia eolica oltre ad avere un basso costo di gestione, è una grande amica dell’ambiente, perché non necessita di nessun’altra risorsa naturale se non il vento stesso.
Questa energia è diversa da quella prodotta da grandi generatori che producono molti gas chimici dannosi per l’aria e causano il surriscaldamento climatico nel mondo.
La mancanza di elettricità ininterrotta nel paese è un problema che riguarda tutti quando indebolisce le proprie attività quotidiane, allora rivolgiamo i rimproveri al governo e vogliamo che trovi un'alternativa per eliminare questo problema.
Parlando con Tanzania Daima nei suoi uffici, che si trovano nelle circoscrizioni della città di Dar es Salaam, il direttore della Società Windpower Technics Tanzania, Amos Makele, dice che sono pronti a diffondere la tecnologia dell’energia eolica nel paese.
Makele dice che questa società è stata fondata nel 2008, ma prima ha fatto ricerche geografiche per 4 anni per arrivare ai livelli necessari per la tecnologia dell’energia eolica.
Dice che i bisogni di energia elettrica per i Tanzaniani sono grandissimi, perciò utilizzare un solo particolare tipo di energia elettrica significa ritardare lo sviluppo di un paese giovane come la Tanzania.
I paesi europei e americani hanno smesso di dipendere dall’energia idrica, invece hanno facilitato la produzione di energia eolica... anche noi, la Tanzania, dobbiamo cambiare imitando questo esempio, dice Makele.
Il loro obiettivo, dice, è far raggiungere questo servizio nelle province e nei villaggi dove il servizio di energia elettrica non è ancora arrivato e perciò dare ai cittadini la possibilità di condurre le loro attività in modo moderno, quando l'elettricità per loro avrà fatto piccolissime modifiche ai piccoli strumenti come le batterie.
Quando la batteria sarà abbandonata, la nostra pala eolica per la produzione di elettricità durerà da 6 a 10 anni prima di una revisione, dice il direttore.
Ha spiegato che l’energia eolica si usa nelle in diverse zone dei paesi europei e americani come strade, campagne, industrie e campi sportivi, perché i suoi costi sono convenienti in confronto all'elettricità di qualsiasi altro tipo del mondo.
Questa tecnologia non necessita di molti cavi, non usa alcun tipo di combustibile, le sue eliche sono fatte girare dal vento produce elettricità che va direttamente in uno strumento chiamato ‘invertitore’ che aumenta l’elettricità fino alla una potenza voluta.
Dentro questo strumento c’è un fusibile corrispondente alla quantità di elettricità e la fa passare nello strumento che controlla le carenze di elettricità, dice Makele.
Makele dice che lo scopo del progetto di produzione di energia eolica, guarda alla comunità Tanzaniana soprattutto nei villaggi, perchè hanno scoperto che gli abitanti dei villaggi non conoscono le possibilità di sviluppo tramite gli strumenti elettrici, situazione che li condiziona economicamente.
Dice che se gli abitanti dei villaggi saranno raggiunti dall’elettricità potranno trattare i loro prodotti dopo averli raccolto e vendere a un buon prezzo, diversamente dal venderli prima di averli trattati.
Dice anche che i villaggi avranno la possibità di vendere bevande fredde.
Parlando della potenza dell’energia eolica, dice ha grandezze diverse a seconda di quanto è grande la pala eolica.
Ad esempio, dice che c’è elettricità di 500, 1 000 Watt e fino a 3 000 Megawatt, a seconda delle destinazioni produttive.
Se è per piccoli consumi di luce, radio e tv, bastano 500 watt... se è necessaria per il frigorifero l’utente deve avere 1 000 watt... ma per le attività industriali deve avere un campo che produca diversi megawatt per avere elettricità assicurata senza rete né bollette mensili dice.
Makele dice che lo scopo di indirizzare i loro sforzi ai villaggi è unirsi agli sforzi del governo per far arrivare l'energia elettrica nei villaggi per facilitare la crescita economica di ogni singolo Tanzaniano o azienda.
Dice che recentemente hanno iniziato ad andare nelle regioni di Dodoma, Singida, Shinyanga e Mwanza per diffondere questi servizi, e dopo la diffonderanno nelle isole di Ukara, Ukerewe, Saanane ecc., l'obiettivo è liberare i residenti dei villaggi dai generatori, che molti di loro usano e che costano tantissimo.
Oltre a questo, Makele consiglia il governo di dare dei sussidi alle società di produzione di energia elettrica affinché siano veloci nella diffusione nei villaggi sebbene ci sia l’Ente per l'Energia nei Villaggi [REA, Regional Energy Authority].
Makele dice che questa tecnologia non è da sottovalutare perché se il governo lo decidesse potrebbe destinare grandi campi all'installazione di pale eoliche e produrre molti megawatt che possono collegarsi alla rete nazionale di distribuzione ed eliminare definitivamente il problema dell’elettricità e della sua distribuzione in tutto il paese.
(
Giovanna Forlenza e Nino Vessella)
|