www.vessella.it www.changamano.org
 

Cerca / Tafuta

Prima pagina / Ukurasa wa kwanza

Se vuoi essere informat@ sugli ultimi articoli pubblicati, iscriviti al nostro NOTIZIARIO, premendo sul pulsante.

Corso di swahili

Vocabolario italiano-swahili

Redazione

Mbatia apigia debe matumizi ya Kiswahili

2008-12-02


Emmanuel Lengwa, Ilala

Tanzania haina lugha maalum ya kufundishia na kutolea elimu inayoweza kuwajenga watoto wa kitanzania kumudu mazingira yanayowazunguka ili kuliletea taifa lao maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho, Ilala Jijini Dar es Salaam.

``Nadhani tuna matatizo makubwa katika mfumo mzima wa elimu hapa nchini. Hilo linajidhihirisha kwa nchi yetu kutokuwa na lugha maalum ya kufundishia, watoto wetu wanafundishwa kwa lugha za kigeni wakati hata lugha ya mama yao wakiwa hawaijui,`` akasema Bw. Mbatia.

Bw. Mbatia amesema kitendo cha Serikali kuruhusu uwekezaji katika sekta ya elimu huku nchi ikiwa haina mfumo thabiti wa elimu na lugha ya kufundishia, kimesababisha hivi sasa shule kuwa na mitaala tofauti na hivyo elimu inayotolewa baina ya shule hizo pia kutofautiana.

``Shule nyingi za wawekezaji binafsi zinafundisha kwa kutumia mitaala ya nchi za nje. Kila mwekezaji wa nje anafundisha mtaala wa nchi aliyotoka. Hata lugha vivyo hivyo, wapo wanafundisha kifaransa, kiarabu, kiingereza na kijerumani... taifa linapotea,``akasema Bw. Mbatia

Akasema athari za nchi kutokuwa na mfumo mzuri wa elimu, hasa wa lugha ya kufundishia, zinaonekana wazi ambapo hata baadhi ya wabunge hawawezi kuzungumza kiswahili fasaha bila ya kuchanganya na lugha za kigeni.

``Hata bunge linaonekana kutokuwa na lugha sahihi ya kuendesha shughuli zake, baadhi ya wabunge hawawezi kuzungumza kiswahili fasaha... hawawezi kujenga hoja bila kutumia lungha ya kigeni,`` akasema

Bw. Mbatia anasema suluhisho la tatizo hilo ili hatimaye nchi iwe na mwelekeo sahihi wa elimu, ni watanzania kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kuwa na mjadala mpana juu ya mstakabali wa elimu ya Tanzania.

Hata hivyo Bw. Mbatia akasema hadi hivi sasa, hakuna nchi hata moja duniani ambayo inafundisha kwa kutumia lugha ya kigeni na hivyo kuitaka Serikali ianzishe mjadala wa kuona uwezekano wa kufundisha shuleni kwa kutumia lugha ya taifa ambayo ni Kiswahili.

Katika mfumo wa elimu wa Tanzania kwa shule za serikali, wanafunzi hufundishwa kwa lugha ya kiswahili na kisha kiingereza hutumika kuanzia sekondari hadi elimu ya juu.

 

Mbatia sollecita l’utilizzo del Kiswahili.

2008-12-02


Emmanuel Lengwa, Ilala

La Tanzania non ha una particolare lingua d'insegnamento e per fornire l'istruzione che può far rafforzare ai bambini tanzaniani il proprio ambiente e portare nel loro paese il progresso.

Questa opinione è stata espressa dal presidente del partito dell'NCCR-Mageuzi, parlando con i giornalisti nella sede centrale del partito, Ilala, in Dar es-Salaam.

"Penso che abbiamo dei grandi problemi nell’intero sistema scolastico nel paese. Ciò che risulta nel nostro Paese dall’assenza di una lingua specifica per l’insegnamento, è che i nostri bambini sono istruiti con lingue straniere mentre non conoscono neppure la lingua delle loro madri”, dice il signor Mbatia.

Il signor Mbatia ha detto che l'azione del governo di permettere investimenti nel settore dell'istruzione non avendo un solido sistema scolastico e una lingua di insegnamento finora ha fatto sì che le scuole abbiano curriculi differenti perciò anche l'insegnamento fornito da queste scuole è differente.

“In molte scuole di investitori privati si insegna usando un curricolo di paesi esteri. Ogni investitore straniero insegna il curricolo del suo paese d'origine. Perfino per la lingua è così, stanno insegnando il francese, l'arabo, l'inglese e il tedesco... la nazione si sta perdendo”, ha continuato il signor Mbatia.

Ha detto che gli effetti per il paese dell'assenza di un buon sistema scolastico, soprattutto di una lingua di insegnamento, appaiano chiaramente quando persino alcuni parlamentari non sanno parlare swahili corretto senza mescolarlo con lingue straniere.

“Persino il Parlamento sembra non avere una lingua corretta per condurre i propri affari, una parte dei parlamentari non sanno parlare in swahili corretto... non sanno preparare una interrogazione senza utilizzare una lingua straniera,” ha detto.

Il signor Mbatia dice che la soluzione a questo problema, affinché finalmente il Paese abbia una direzione corretta dell'istruzione, è che i tanzaniani stessi si siedano attorno a un tavolo affinché ci sia un'ampia discussione sul futuro dell'istruzione in Tanzania.

Quindi il signor Mbatia dice che in finora, non c'è alcun Paese al mondo che insegni con l'utilizzo di una lingua straniera e per questo vuole che il governo inizi una discussione per trovare la possibilità di insegnare a scuola con l'utilizzo della lingua nazionale che è il swahili.

Nel sistema scolastico della Tanzania nelle scuole statale gli studenti sono istruiti con il swahili e infine l'inglese è usato dalla secondaria fino all'istruzione superiore.

( Giovanna Forlenza e Nino Vessella)

Changamano ONLUS (www.changamano.org).

© Nino Vessella, 2003-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.